Sijaona Mwanaume Mwingine Aliyestaili Kuwa Mume Wangu Ila Bila Chid Mapenzi Mingedondoka- Shamsa Ford

Sijaona Mwanaume Mwingine Aliyestaili Kuwa Mume Wangu Ila Bila Chid Mapenzi Mingedondoka- Shamsa Ford
STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameweka wazi kuwa kama isingekuwa mumewe Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ kumuweka ndani huenda hadi leo angekuwa amedoda kwa kitoolewa kwani kwenye ulimwengu huu haoni kama kuna mwanaume aliyestahili kuwa mumewe.



Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alisema kuna sababu nyingi za kumfanya aseme hivyo kubwa ikiwa ni jinsi mwanaume huyo anavyompenda kwa dhati kiasi kwamba anaamini ame­letwa na Mungu spesho kwa ajili yake.



“Hata kama dunia ingeisha leo na tukarudi mara ya pili mimi bado nin­gemchagua mume wangu Chid kwa sababu naona ndiye mwanaume pekee aliyekuja kwa ajili yangu. Ananipa furaha isiyo kifani kiasi kwamba naamini kama asingetokea yeye, mpaka leo ningekuwa sijaolewa, yaani ningekuwa bado nas­ubiri aje hata angechelewa vipi,” alisema Shamsa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad