Simba Wavunja Rekodi Yao

Simba Wavunja Rekodi Yao
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, wamevunja rekodi waliyoiweka msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo 14 ya kwanza.



Msimu uliopita Simba baada ya kucheza michezo 14, ilikuwa imejikusanyia pointi 32 ambazo msimu huu imezivuka. Hivi sasa timu hiyo ina pointi 33 katika mechi 14.



Kwa upande wa mabao ya kufunga, katika mechi 14 ambazo ni sawa na za msimu uliopita, Simba hivi sasa inayo 28
wakati msimu uliopita ilikuwa nayo 31.



Katika kupoteza, hivi sasa imepoteza mechi moja na msimu uliopita ilikuwa haijapoteza. Mabao ya kufungwa, msimu uliopita ilikuwa imefungwa mabao sita, lakini msimu huu wameimarisha safu yao ya ulinzi na wamefungwa mabao matano.



Kwa upande wa nafasi, msimu uliopita kipindi kama hiki Simba walikuwa wanaongoza ligi, lakini kwa sasa wapo nafasi ya tatu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad