Klabu ya Simba imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Waliofunga penalti za Simba SC ni mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi, mabeki Mghana, Nicholas Gyan, Muivory Coast, Serge Wawa, kipa mzawa Deogratias Munishi ‘Dida’ na kiungo Mzambia, Clatous Chama.
Kwa upande wa Mbao FC waliofunga ni Said Khamis, Peter Mwangosi na Vincent Philipo huku Rajesh Kotecha akipiga juu ya lango.