Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwenda gerezani kumhoji mshtakiwa wa pili Alloycious Mandago katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh2bilioni.
Wakili wa Takukuru Leonard Swai ameeleza hayo jana Alhamisi, Januari 24, 2018 mbele ya hakimu mkazi mkuu Thomasi Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Swai alidai kesi hiyo iko hatua za mwisho kwa ajili ya kuandaa maelezo lakini wanaombi kwa ajili ya kumhoji mshtakiwa wa pili akiwa magereza.
Mahakama iliridhia mshtakiwa huyo kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Mandago, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Mohamed Yusufali na Isaac Kasanga ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 39 likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya Sh2 bilioni.
Takukuru Yaiomba Mahakamani kumuhoji Mtuhumiwa Gerezani
0
January 25, 2019
Tags