TFF Yapata Pigo Mwenyekiti Wake Afariki Dunia

TFF Yapata Pigo Mwenyekiti Wake Afariki Dunia
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya  Maadili ya shirikisho la soka nchini (TFF), Hamidu Mbwezeleni, amefariki dunia leo Januari 16, 2019 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.


Taarifa ya TFF imeeleza kuwa Rais Wallace Karia amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa kiongozi huyo ambaye amedai alikuwa ni mfano wa kuigwa. Pia Karia ametoa pole kwa familia ya Mbwezeleni na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla.

Maisha ya Mbwezeleni Ndani ya TFF

Kiongozi huyo aliingia ndani ya TFF mwezi Septemba 2013, alipoteuliwa na Rais wa TFF kwa wakati huo ndugu Leodgar Tenga kuwa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo.

Katika kamati hiyo Mbwezeleni alifanya kazi na wajumbe kama Moses Kaluwa ambaye alikuwa makamu mwenyekiti pamoja na wengine kama Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.

Mnano mwezi Agosti 2017, Rais Karia akiwa madarakani alimteua Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Maadili kamati ambayo ilikuwa na Makamu Mwenyekiti, Wakili Steven Zangira wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.

Hata hivyo Mbwezeleni anakumbukwa kwa maamuzi yake ya kamati yake ambayo mara nyingi alikuwa akiyasoma yeye na kuzua mijadala mbalimbali.

Moja ya kumbukumbu hiyo ni pale alipotangaza kumfungia maisha Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF wakili msomi Revocatus Kuuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad