TFF yatangaza sifa za mpiga kura uchaguzi Yanga

TFF yatangaza sifa za mpira kura uchaguzi YangaMwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela, amezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa Yanga kwa kuwataka wagombea kufanya kampeni kwa amani bila kumchafua mwingine

Akiongea leo kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa Yanga Malangwe amesema mgombea anaruhusiwa kujinadi kokote ikiwemo katika tawi lolote la Young Africans.

''Kampeni zinatakiwa ziwe za kisataarabu sio kusemeana maneno yasiyofaa, pia wanachama wote wenye kadi za kitabu na zile za benki wataruhusiwa kupiga kura ilimradi tu ziwe zimeahakikiwa'', amesema.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Young Africans ambaye pia ni Msaidizi wa Kaimu Mwenyekiti Siza Lyimo, amewataka Wanachama kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo utakaokuwa wa amani na utulivu.

Uchaguzi huo utafanyika Jumapili Januari 13, 2019 kwenye ukumbi wa bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay Dar es salaa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad