Trump Asalimu Amri....Serikali ya Marekani Yafunguliwa




Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kufunguliwa kwa idara za serikali kuu ambazo zilifungwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, baada ya kufikia makubaliano na kamati ya pamoja ya bunge.

Makubaliano yaliyofikiwa Ijumaa yataruhusu idara za serikali kuu kufunguliwa kwa kipindi cha wiki tatu mpaka Februari 15 wakati ambapo majadiliano yataendelea kufanyika kuhusu suala kuu la ulinzi wa mpaka.

Vyanzo vya habari katika Bunge la Marekani - Congress vinasema kuwa .Makubaliano yaliyofikiwa hayajumuishi fedha za ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

Rais Donald Trump amesaini makubaliano ya kufungua tena serikali ya Marekani kwa kipindi cha wiki tatu; baada ya kuvunja rikodi ya kufungwa idara hizo za serikali kuu kwa muda mrefu kuliko wakati wowote.

Rais Trump amesema kuwa mkataba huo uliofikiwa utaiwezesha serikali kuendesha shughuli zake hadi Februari 15.

Amesema kuwa wafanyakazi wa serikali kuu watalipwa mshahara wao wote "kwa haraka iwezekanavyo."

Akizungumza akiwa White House, Rais Trump amesema makubaliano yamebainisha kuwa wanaweza kuelewana kwa ajili ya maslahi ya taifa la Marekani na watu wake.

Amesisitiza umuhimu wa ulinzi wa mpaka ili kuzuia uhamiaji haramu pamoja na uingiaji wa madawa ndani ya ardhi ya Marekani.

Trump amesema wajibu na kipaumbele chake cha juu ni kuilinda nchi na kulinda wamarekani wasiingiliwe na watu ambao ni wabaya na kuongezea kuwa Marekani inapenda kukaribisha wageni kutoka kile pembe ya dunia, lakini waingie kwa utaratibu unaotakiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad