Tundu LISSU Ataki MCHEZO Kabisa..Atarajia Kuanza Ziara Marekani na Ulaya



Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia Jumatatu, Januari 28, mwaka huu, ambako mbali ya kufanya vikao kadhaa na viongozi wa kiserikali na jumuiya mbalimbali, pia atapata fursa ya kutoa mihadhara ya kitaaluma na kufanya mahojiano na vyombo vya habari.

Siku hiyo ya kwanza ya ziara yake, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, atakuwa nchini Ujerumani kwa siku mbili, ambako atakutana na baadhi ya maofisa wa Serikali pamoja na wabunge wa Bunge la Ujerumani.

Baadae Lissu atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji ambako atakutana na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, wabunge wa EU pamoja na wanadiplomasia wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao EU.

Baada ya Ubelgiji,  Lissu ataelekea Washington DC, Marekani kwa siku 10 ambapo mbali ya kukutana na Watanzania wanaoishi nchini humo, hususani katika maeneo ya Washington, Houston, Texas, Birmingham na Alabama, atakutana pia na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na  Watendaji wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID). Halikadhalika atakutana na Kamati za mabunge yote mawili ya Marekani zinazohusika na Uhusiano wa Nje (Afrika).

Katika ziara hiyo, Lissu atapata fursa ya kuwasilisha mada juu ya masuala mbalimbali katika taasisi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na Center for Strategic and International Studies (CSIS) na The Atlantic Council and the World Resources Institute (WRI). Mhe. Lissu ana historia na taasisi ya WRI kwani aliwahi kuwa mmoja wa watafiti wake miaka ishirini iliyopita.

Akiwa mjini Washington DC, Lissu atakutana na kufanya mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vilivyoko Mji Mkuu wa Marekani.

Lissu atahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mhadhara mkubwa wa umma katika Chuo Kikuu cha George Washington (GWU). Chuo hicho ni moja ya taasisi kongwe na kubwa za elimu ya juu nchini humo na duniani kwa ujumla.

Kutokana na umuhimu wa ziara hiyo kwa Chama, siasa za Tanzania na mapambano ya kutafuta mabadiliko ya kweli nchini kwa ujumla, siku ya Jumapili, Januari 27, mwaka huu, Mhe. Lissu atazungumzia baadhi ya masuala kuhusu ziara hiyo pamoja na maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake.

Imetolewa leo Jumamosi, Januari 26, 2019 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. I guess when ccm hear this, they won't sleep the whole night for fearing what Tundu Lissu is going to talk with those people.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, you are totally wrong...!!!
      Lizzu ni sisimizi nna CMM ni Tembo wapi na wapi au na weeukokatika njama ya kumvua uenyekiti Mtowe..??
      Lizzu ni Kibaraka aliepona na anaenda tembeza Koia apate Ruzuku na kujieleza kutofanikisha ahadi zale kwa Mabepari na Walowezi aliokula pesa zao aMaka8kia bado tunayo na tutaendelea kuwa nayo a Ndege zetu zinaendeea kuja na ata kibaraka mwenzae anajitahidina ukweli ndio huo au vipi baba twita fezi buku Jitto upo mwaya.
      Mawwese debe kiasi gani kwa beiya sasa Jan 2019.??

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad