UDSM Watishia Kuingia Mgogoro na Serikali Kisa Hiki Hapa

UDSM Watishia Kuingia Mgogoro na Serikali Kisa Hiki Hapa
JUMUIYA ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), imesema watalazimika kuingia katika mgogoro na serikali, ikiwa haitawalipa madai yao ya muda mrefu kufikia mwishoni mwa mwezi huo.



Jumuiya hiyo imedai wanachama wake wanaidai serikali za Sh. bilioni 11 kutokana na malimbikizo ya posho ya nyumba ya kuishi na nyongeza ya mishahara. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Udasa, Dk. George Kahangwa, alidai wamekuwa wakidai stahiki hizo kwa muda mrefu bila mafanikio.



“Kwa wanataaluma wa UDSM kwa mfano, hadi sasa wanadai kutoka serikalini jumla ya Sh. bilioni 6.272, ikiwa ni deni la kuanzia Januari 2014 hadi Septemba mwaka jana. Pesa nyingine ni Sh. bilioni tano ambazo ni nyongeza ya mishahara iliyotokana na msawazisho wa utaratibu wa utumishi katika vyuo vya umma,” alisema Dk. Kahangwa.



“Mwaka jana, Ofisi ya Utumishi wa Umma ilituahidi kwamba serikali ingetulipa madai hayo kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha wa 2017/2018, ilipofika Juni ni wana Udasa 102 tu na wengine wachache kutoka vyuo vikuu vingine ndiyo walilipwa, lakini 1,060 waliendelea kusubiri mpaka leo (jana).”



Dk. Kahangwa alisema Udasa pia inadai mishahara ya miezi mitano ya wanataaluma wapya walioajiriwa mwaka 2017 pamoja na nyongeza ya mshahara za kila mwaka na kifuta jasho kwa wastaafu walioko katika mikataba ya kazi na kwamba baadhi ya wastaafu hao wameondoka kazini bila kulipwa hazi zao hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad