Katika tamko lililotolewa jana baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian alisema Fayulu, ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili, ndiye aliyetakiwa kutangazwa mshindi.
"Kwa kweli inaonekana matokeo yaliyotangazwa, hayaendani na matokeo halisi," alisema alipozungumza na kituo cha televisheni cha CNews.
"Kwa kuangalia (matokeo halisi), Fayulu ndiye kiongozi aliyepatikana katika uchaguzi huu. "
Alisema Kanisa Katoliki, ambalo lina wafuasi wengi na ambalo lilituma waangalizi 40,000, linajua nani hasa aliyehinda na maoni yao yanaonyesha mshindi ni Fayulu.
"CENCO ilifanya ukaguzi na kutangaza matokeo ambayo yalikuwa tofauti," alisema akimaanisha baraza la maaskofu la Kanisa Katoliki.