Ukaribu wa Lynn na Sheta Mmh! Mwenyewe Afunguka A-Z

Ukaribu wa Lynn na Sheta Mmh! Mwenyewe Afunguka A-Z
KUTOKANA na hivi karibuni kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanatoka kimapenzi, muuza nyago maarufu Bongo ambaye kwa sasa amejiingiza rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Irene Godfrey ‘Lynn’ ameibuka na kufungukia ukaribu wake na mwanamuziki Nurdin Bilal ‘Shetta’ wakiwa Afrika Kusini ‘Sauz’. 



Lynn aliieleza Risasi Jumamosi kuwa ukaribu wake na Shetta unatokana na kazi wanayoifanya kwa pamoja lakini alishangazwa na maneno kwamba wanatoka kimapenzi kitu ambacho siyo kweli.



“Hivi naanzaje kutoka na Shetta jamani kwa hiyo kila mtu nitakayekuwa naye karibu ni bwana wangu? Shetta ni mshikaji wangu, siwezi kutoka naye na huku Afrika Kusini tumekuja kikazi wala siyo kula bata kama watu wanavyosema ila kwa kuwa wanapenda kutunga uongo waendelee tu kuamini, sina muda wa kuwalazimisha waelewe, napiga kazi tu,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad