Umoja wa Afrika, Marekani Walaani Shambulio la Hoteli ya Kifahari Jijini Nairobi

Umoja wa Afrika, Marekani walaani shambulio la hoteli ya kifahari jijini Nairobi
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio la Hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.

Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za uokozi wa raia na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo. Pia amesema tukio hilo linaonesha umuhimu wa kupitia upya mipango ya kuongeza nguvu ya kupambana na vikundi vya kigaidi barani Afrika.

"Mwenyekiti wa Kamisheni anathibitisha utayari wa AU kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Nchi Wanachama katika kupambana na visa vya ugaidi pamoja na harakati za kutuliza hali nchini Somalia na mapambano dhidi ya kundi al-Shabaab kupitia vikosi vyake vya AMISOM.

Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Kenya Bw Robert Godec ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad