Unakumbuka Video ya Trafiki Wakimpiga Dereva wa Lori..Kangi Lugola Atoa Maagizo


Wakati video inayoonyesha askari watatu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakimshambulia dereva wa lori ikizua mjadala mitandaoni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limesema litatoa tamko la tukio hilo haraka iwezekanavyo.

Katika video hiyo, askari hao wanuaonekana wakimshambulia dereva huyo kabla ya kundi la wananchi waliokuwa wakiwashangaa awali, kuamua ugomvi huo.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alisema, “Nimemtumia kipande hicho cha video Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimu ili afuatilie kujua undani wake na taarifa itatolewa.”

Hata hivyo, alipotafutwa kwa simu jana, Kamanda Muslimu hakupatikana kwani simu yake iliita bila kupokewa.

Lakini akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange alisema tayari wameshapewa maelezo na watatoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo.

“Mimi mambo yote huwa yanatolewa ofisini kwa njia ya ‘Press’ (mkutano na waandishi wa habari) sio kwa njia ya simu hivyo mtafahamu ni kitu gani,” alisema.

Tukio hilo limeibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii kutokana na jinsi askari hao walivyotumia nguvu kubwa kumkamata dereva huyo ambaye haikufahamika mara kosa alilotendana alikokuwa akitokea au kuelekea.

Katika video hiyo, askari wanaonekana wakimshambulia dereva huyu katika jitihada za kutaka kumkamata na kumdhibiti lakini alionekana kufanikiwa kujinasua katika mikono yao.

Katika patashika hiyo, dereva huyo anasikika akipiga kelele kuomba msaada akilalamika kung’atwa shingoni na mmoja wa askari.

Baada ya kufanikiwa kutoka katika mikono ya askari dereva wa lori alionekana kukimbilia katika gari na kuchukua panga jambo ambalo liliwafanya watu kutimua mbio.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad