Uongozi wa Simba SC umefunguka Baada ya kichapo cha mabao 5-0 na AS Vita katika mchezo wao wa hivi karibuni wa Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi pamoja na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Bandari kwenye michuano ya SportPesa Cup na kusema kuwa bado wana imani na kocha Patrick Aussems hivyo mashabiki wapunguze jazba.
Simba katika mashindano matatu ambayo wameshiriki yote hawana uwezo wa kutwaa kombe kutokana na kutolewa mapema ikiwa ni pamoja na lile la FA, Mapinduzi waliishia fainali na kombe la SportPesa ambalo leo wanapigania nafasi ya tatu na Mbao FC.
Ofisa Habari wa Simba , Haji Manara amesema katika mkataba wa mbelgiji Aussems hakuna makubaliano juu ya makombe mengine zaidi ya kombe moja na sharti moja ambalo amelitimiza tayari.
"Kwenye mkataba wa Aussems tumemwambia kwamba tunahitaji atufikishe hatua ya makundi Afrika jambo ambalo amefanikiwa kulifanya na lipo kwenye mkataba pamoja na kutupatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao upo mikononi mwetu.
Hata hivyo amesema makombe mengine hawajayaweka kwenye makubaliano wanayoshiriki kulinda heshima na wakifanikiwa kuyapata ni jambo jema hivyo na kushindwa kuyapata kwao haina maana kwamba Kocha hafai hapana wanamipango yao na wanafanya kazi kwa utaratibu.