URUSI: Wanasayansi Waliogundua Bomu Linaloenda Kwa Kasi zaidi Duniani Wakamatwa, Watuhumiwa Kwa Uhaini

MOSCOW: Rais wa Urusi, Vladimir Putin amekuwa mara kwa mara akitamba kuhusu silaha zake mpya za 'Hypersonic' zinazodaiwa kwenda kwa kasi ya mara 20 zaidi ya kasi ya sauti. Mara kwa mara Rais Putin amekuwa akiikumbusha Dunia kuhusu umahiri wa silaha hizo na kwamba ni za kipekee na kuwa hakuna nchi nyingine yenye silaha za uwezo huo isipokuwa Urusi pekee.

Lakini, wakati Putin akiwasifia wanasayansi na wataalamu waliofanikisha kuundwa kwa silaha hizo, amekuwa akisita kusema kuwa baadhi ya wataalamu wa juu zaidi katika mpango huo wa 'Hypersonic Missile' wapo gerezani wakichunguzwa dhidi ya uhaini kutokana na kuvujisha taarifa kwa washirika wao wa nje ambao wanatajwa kuwa ni maadui wa Urusi.

Mamlaka ya usalama ya FSB inawatuhumu watu 10 kwa kosa la kuvujisha taarifa za juu za siri kuhusiana na silaha za 'Hypersonic' kwa NATO.

Mmoja wa watuhumiwa ni mmoja wa wanataaluma viongozi katika Roskosmos, Viktor Kudryavtsev ambaye anatuhumiwa kuvujisha taarifa za siri kwenda moja ya nchi za NATO, taarifa ambazo zinahusiana na teknolojia ya 'Hypersonic' iliyotumika kwenye kombora la Kh-47M2 “Kinzhal” pia kuvujisha taarifa zingine kuhusiana na “Avangard,” ambao ni mfumo uliofanyiwa majaribio Jumatano ya tarehe 2 January Mwaka 2019. Kuendana na makosa hayo, Bw. Kudryavtsev ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo anaweza tumikia kifungo cha hadi miaka 20 jela.

Mwaka mmoja kabla ya kukamatwa kwake Bw. Viktor Kudryavtsev, alipiga kampeni ya kuachiliwa huru kwa mwenzake katika kitengo cha TsNIIMash ndani ya Roskosmos, Bw. Vladimir Lapygin, mwenye miaka 76, mtaalamu wa vyombo vya usafiri vya anga 'Spacecrafts' ambaye alifungwa miaka 7 jela kwa madai ya uhaini kutokana na taarifa za siri za serikali zilizovuja kwenda China.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad