VIDEO: Hii ndio Sababu ya 50 Cent Kununua Ticket 200 Kwenye Show ya Ja Rule


Rapper 50 Cent amefunguka kwenye mahojiano ya kipindi cha “The Late show” na mtangazaji Stephen Colbert na kusema alikuwa akipima uwezo wa Ja Rule kufanya show bila uwepo wa watu 200 mbele yake.

Mwezi October 2018 50 Cent alinunua tiketi 200 za siti zote za mbele katika ukumbi ambao Ja Rule alitakiwa kufanya show ambapo ticket moja ilikuwa ikigharimu dola 15 za Kimarekani sawa na elfu 34 za Kitanzania na hivyo ilimgharimu 50 Cent Milioni 9 za Kitanzania kununua tiketi 200.

50 Cent alisema “Sasa tunakupima uwezo wako katika tamasha, pale unapokuja na unakuta hakuna watu kwenye siti za mbele, inabidi uendelee kutumbuiza kama vile kuna watu”

Bifu kati ya 50 Cent na Ja Rule linatajwa kuwa la muda mrefu tokea mwaka 1999 na hawajawahi kurekebisha tofauti zao mpaka leo hii, hivyo ni wazi bifu lao linaingia mwaka wa 20 sasa toka watofautiane 1999.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad