VIDEO: RC Gambo Abaini Madudu Yanayofanyika Mauaji ya Twiga



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea Taarifa ya kamati maalumu iliyohusisha watu kutoka kada mbalimbali aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza  mauaji ya wanyama pori hasa Twiga wilayani Longido mkoani Arusha katika kipindi cha miaka miwili.


Akizungumza na wanahabri ofisini kwake Leo Gambo amesema baada ya kamati hiyo kufanya uchunguzi  wa kina ilibaini kuwa katika kipindi cha miaka miwili  2017/2018; jumla ya Twiga 35 walikufa kutokana na sababu mbalimbali lakini Twiga ambao walikufa kutokana na sababu za ujangili ni 25

Gambo amesema Kamati hiyo imegundua kwamba moja ya sababu ambazo zinachangia ujangili wa Twiga kuongezeka kuwa ni pamoja na sababu za kibiashara; ambapo kamati hiyo ilipata taarifa ya watu wasiopungua 25 ambao wanatajwa kuhusika na masuala ya ujangili Wilayani Longido.

Aidha Gambo ameiomba wizara ya maliasili na Utalii kuunda Timu ya uchunguzi kuhusu malalamiko dhidi ya Kampuni ya Uwindaji ya Green Milles kuhusiana na kitalu kudaiwa na vijiji vinavyopakana kutotengeneza miundombinu ya barabara na kutofanya doria kwenye kitalu chake..

Kaimu kamanda Mkoa wa Arusha kamishna msaidiz Longinus Tibishubwamu Amesema mpaka sasa Jeshi hilo linawashikilia Watu 5 huku wakiendelea kuwafatilia wengine 20 ambao wametorokea Nchi jirani ya Kenya nakusisitza kuwa Watu hao Wanawatia Nguvuni

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad