Vyama 8 vya Upinzani Vyafurahia Kesi ya Zitto Kabwe Kufutwa

Vyama 8 vya Upinzani Vyafurahia Kesi ya Zitto Kabwe Kufutwa
Vyama vinane visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu kulifuta shauri lililofunguliwa na baadhi ya wanasiasa kupinga Bunge kujadili muswada wa marekebisho wa sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2018.

Tamko la vyama hivyo lililotolewa  jana Jumatatu Januari 15, 2019 limeeleza uamuzi huo wa Mahakama ni mzuri na umetenda haki kwa vyama vya siasa ambavyo vilidai sheria hiyo.

Vilevile vyama hivyo ambavyo ni DP, AAFP, Demokrasia makini, SAU, TLP, UDP, NRA, UMD vimempongeza Spika Job Ndugai kwa kualika kila chama kwa ajili ya kutoa maoni yao kuhusu muswada huo mbele ya kamati.

Akisoma tamko hilo, Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya alisema kwa upande wao maboresho ya sheria hiyo wanayaunga mkono kwa asilimia 100 kwa kile alichodai ndio hitaji lao.

“Spika amefanya jambo jema sana kutuhusisha vyama katika hilo na tutakwenda kupeleka maoni yetu kadri tutakavyoona inafaa,” alisema Mluya.

“Tunaamini kamati iko vizuri itayachambua yote maana tutaeleza hata yale yanayoonekana hayafai,” alisema Mluya.

Mluya alisema suala kubwa ambalo wamelifurahia katika muswada huo ni kuondolewa kwa vikundi vya ulinzi na usalama ndani ya vyama na jukumu hilo kubaki mikononi mwa Serikali.

Naye Katibu Mkuu wa NRA, Hassan Almas aliyeeleza kufurahishwa kwake na kifungu hicho alisema, “Sheria imetutendea haki sisi ambao vyama vyetu havikuwa na uwezo wa kumiliki jeshi au vikundi vya ulinzi. Kuna watu wanajiita makamanda na wana vyeo baada ya kupewa mafunzo ya kijeshi hii ilikuwa hatari.”

“Kwani kuna haja gani ya chama kuwa na jeshi au kikundi cha ulinzi wakati wote tunatakiwa kuwania dola itakayotuwezesha kuongoza majeshi yote. Uchaguzi ukiisha aliyeshinda ndiye anakuwa kiongozi wa majeshi yote yaliyo chini ya Serikali,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa (AAFP) Rashid Rai alisema fursa hiyo waliyopewa na Spika wataitumia vizuri na kushiriki kutoa maoni kuhusu muswada huo.

“Spika amefanya jambo jema sana kutuhusisha vyama katika hilo na tutakwenda kupeleka maoni yetu kadri tutakavyoona inafaa. Tunaamini kamati iko vizuri itayachambua yote maana tutaeleza hata yale yanayoonekana hayafai,”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad