Walichosema TFF kuhusu Tanzania kufutiwa uenyeji wa AFCON U17
0
January 26, 2019
Baraza la wadhamini wa shirikisho la soka nchini TFF limesema maswala ya kimichezo kupelekwa mahakamani kutasababisha Tanzania kufutiwa uenyeji wa mashindano ya AFCON U17 yanayotarajiwa kufanyika hapa nchini baadae mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ammy Ninje akiwa nchini Misri kwenye semina ya wakurugenzi.
Akizungumza na wanahabari leo Mwenyekiti wa baraza hilo Leodgar Tenga amesema kuwa suala la aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura kwenda mahakamani linahitaji kumalizwa mapema kwa kutumia busara ili lisiwe na athari kwenye uandaaji wa michuano hiyo.
''Busara ya watanzania itumike ili kulimaliza mapema kwani hili vinginevyo ni jambo ambalo linaweza kugharimu taifa kwa kufutiwa uenyeji wa AFCON U17 ambayo inaanza mwezi April'', amesema Tenga.
Kwa upande mwingine baraza hilo limeunga mkono jitihada na mafanikio ya shirikisho la soka nchini TFF ambayo yameipatia heshima nchi licha ya timu ya taifa kusuasua.
Wiki hii shirikisho la soka nchini liliweka wazi barua iliyotumwa na FIFA ya kumfungia Waambura kutojihusisha na maswala ya soka huku likiwaonya wanachama wake kutopelekea maswala ya soka mahakamani kwani ni kinyume na katiba ya TFF, CAF na FIFA.