Idadi ya watu waliofariki katika shambulio la wanamgambo wa Somalia, walipoivamia hoteli moja mjini Nairobi imeongezeka hadi 21 kwa mujibu wa serikali.
Mamia ya watu walilazimika kutoroka umwagikaji damu ulioshuhudiwa katika hoteli ya DusitD2 na jengo la kibiashara siku ya Jumanne, Watu 28 waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali, huku wengine 19 wakiwa hawajulikani waliko, shirika la msalaba mwekundu linasema.
Kundi lililoko nchini Somalia al-Shabab limekiri kuhusika na shambulio hilo, lililozusha operesheni ya saa 19 ya kiusalama, Kenya imekuwa ikilengwa na kundi la al Shabab tangu Okotoba 2011, wakati taifa hilo lilipotuma vikosi vyake nchini Somalia kupambana na kundi hilo la jihadi.
Rais Uhuru Kenyatta Jana Jumatano alitangaza kwamba washambuliaji hao wameangamizwa na kwamba operesheni ya uokozi imekamilika.
Miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo ni pamoja na mmoja aliyeponea shambulio la kigaidi la 9/11 , Shabiki sugu wa soka, na marafiki wawili wa dhati.