Wamarekani weusi wasio kuwa na hatia waombwa radhi baada ya miaka 70


Mkuu wa polisi Kaunti ya Lake Willis McCall, mwanzo kushoto, na mtu ambaye hakutambuliwa wamesimama pembeni ya Walter Irvin, Samuel Shepherd and Charles Greenlee, kutoka kushoto huko Florida. Watu hao walituhumiwa na kosa la kubaka 1949.

Wamarekani weusi wanne waliokuwa hawana hatia ambao walituhumiwa kwa kosa la kumbaka msichana wa kizungu mwenye umri wa miaka 17 kusini mwa jimbo la Florida Marekani miaka 70 iliyopita familia zao ziliombwa radhi familia kwa niaba yao Ijumaa.

Charles Greenlee, Walter Irvin, Samuel Shepherd na Ernest Thomas walikuja kujulikana kwa jina la Groveland Four. Wote wanne ni marehemu. Lakini ndugu wa familia hizo bado wako hai.

Familia hizo zilihudhuria usikilizwaji wa shauri hilo ili kuwasafisha watu hao kutokana na tuhuma hizo, huko Tallahassee Ijumaa ambapo maafisa walipiga kura ya pamoja kuwaomba radhi watu hao wanne.

“Kitendo hiki sahihi cha kuwaomba radhi hakijachelewa kabisa,” Gavana Ron DeSantis amesema katika tamko lake. “Naamini kuwa utawala wa sheria ndio jambo tukufu linalo iunganisha jamii. Wakati inapokanyagwa, sote tunaathirika. Kwa hawa vijana wanne maarufu kama Groveland Four, ukweli ulikuwa umefichwa.”

Thomas aliuliwa na kundi lenye mhemuko muda mfupi baada ya tukio hilo 1949.

Wengine watatu waliteswa na hatimaye kukiri makossa na kuhukumiwa na washauri wa mahakama ambao wote walikuwa ni wazungu.

Shepherd alipigwa risasi na kuuliwa na mkuu wa polisi wa eneo ambaye alikuwa anapeleka kuhudhuria kesi iliyo kuwa inarudiwa tena. Greenlee na Irvin walihukumiwa kifungo cha maisha.

Norma Padgett ambaye ilikuwa inadaiwa amebakwa, bado yuko hai. Yeye pia alihudhuria siku ya Ijumaa kikao hicho.

“Mimi siyo muongo,” amesema kukiambia kikao hicho.

Wachunguzi wa kujitegemea wamethibitisha kuwa watu hao ambao walihukumiwa bila ya ushahidi, wakati wa zama za uovu wa nadharia iliyojulikana kama Jim Crow nchini Marekani, walikuwa hawana hatia kutokana na tuhuma hizo. Zama hizo zilikuwa ni zenye sera za ubaguzi na ukandamizaji na pia ulikuwa unataka kuendelea utumwa.

Devil In The Grove, ni kitabu kilicho andikwa juu ya kesi ya Groveland Four, na kushinda tuzo ya Pulitzer Prize mwaka 2013.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad