Wamiliki wa Mabenki Wataja Sababu za Kutowakopesha Wachimba Madini

Wamiliki wa Mabenki Wataja Sababu za Kutowakopesha Wachimba Madini
Mwenyekiti wa umoja wa mabenki Tanzania, Abdulmajid Nsekela amesema benki zimekuwa zikishindwa kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo kutokana na ukosefu wa leseni na wengine kukodisha jambo ambalo linawafanya washindwe kutambua uhalali wao.

Nsekela ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB alisema hayo jana katika mkutano wa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais John Magufuli.

 “Wachimbaji hao wamekuwa wakishindwa kufanya upembuzi yakinifu wa mapato yao ambao husaidia benki kutathimini wanachozalisha ili waweze kukopeshwa.”

“Wamekosa mshikamano na umoja ambao ukitiliwa mkazo utaleta matokeo chanya lakini pia wamekuwa wakihamahama jambo ambalo huweka ugumu kwa mabenki kufuatilia utendaji wao,” alisema.

Alisema  kutokana na idadi ya benki kuongezeka amana pia imeongezeka hadi kufikia Sh29.9 trilioni kutoka Sh19.5 trilioni mwaka 2013 hivyo kuwezesha benki hizo kuendelea kufanya vizuri.

Alisema kutokana na kabadilika kwa sera za uendeshaji wa benki hizi sasa watajikita zaidi katika shughuli za kiuchumi na sekta ya madini.

“Mabenki yamekuwa yakishiriki katika sekta ya madini katika njia mbalimbali ikiwamo kutoa mikopo kwa wachimbaji mmoja mmoja na wakandarasi na kushiriki katika shughuli mbalimbali,” alisema

“Salio la mikopo iliyotolewa limezidi kukua kutoka Sh306 bilioni 2016 hadi kufikia Sh357 bilioni katika mwaka 2018 huku makubaliano yakiwa ni kupelekwa katika shughuli za madini tu,” alisema.

Alisema uzalishaji wa wachimbaji wadogo umekuwa duni kwa muda mrefu kutokana na kukosa nyenzo, mitaji jambo ambalo limefanya washindwe kutoa mchango unaostahili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad