Baada ya hapo jana Jumatatu, Januari 7 maafisa kadhaa wa jeshi la Gabon kujaribu kufanya mapinduzi, vyombo vya usalama nchini humo vimefanikiwa kuzima jaribio hilo.
Ripoti za mtandao wa RFI zinasema kuwa kiongozi wa wanajeshi walioshiriki jaribio hilo amekamatwa na wengine wawili wameuawa.
Jaribio hilo limekemewa vikali na viongozi wa umoja wa Afrika, umoja wa Ulaya na umoja wa Mataifa ambao wamesema hakuna demokrasia itakayopatikana kwa nguvu ya kijeshi au kupitia mapinduzi.
Msemaji wa Serikali ya Gabon, Guy Betrand Mapangou amesema kuwa hali ya utulivu imerejea hivi sasa nchini humo, huku usalama ukiwa umeimarishwa kwenye maeneo mengi ya nchi.
Balozi wa Gabon nchini Ufaransa, Flavien Enongoue, amesema uchunguzi tayari umeanza kubaini wanajeshi wengine zaidi waliohusika kupanga na kutekeleza jaribio hilo.
Jaribio hilo limefanyika wakati Rais wa nchi hiyo, Ali Bongo akiwa nchini Moroco ambako anapatiwa matibabu kwa zaidi ya miezi miwili sasa tangu aanze kuugua akiwa nchini Saudi Arabia.
Ali Bongo alianza kuongoza nchi hiyo kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa madarakani kwa miaka 41, alichaguliwa kuendelea na uongozi wa taifa hilo mwezi Agosti mwaka 2009. Siku chache baada ya uchaguzi uliyofanyika Agosti 30 mwaka 2009 alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata 42% ya kura.
Wanajeshi wa Gabon Waliofariki Jaribio la Kupindua Nchi Wadakwa
0
January 08, 2019
Tags