Washukiwa Watano wa Shambulio la Dusit Kenya Wafikishwa Mahakamani Wakificha Nyuso zao

Washukiwa Watano wa Shambulio la Dusit Kenya Wafikishwa Mahakamani Wakificha Nyuso zao
Washukiwa watano wanaohusishwa na shambulio la Jumanne la hoteli ya Dusit mjini Nairobi wamewasilishwa mahakamani .

Watano hao ni pamoja na raia mmoja wa Canada.

Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuwaweka rumande kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea.

Takriban watu 21 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia hoteli ya DusitD2 .


Wanaume wanne walisimamishwa kizimbani katika mahakama kuu jijini Nairobi huku wakificha nyuso zao.

Ni washukiwa wa kwanza kuwasilishwa mahakamani wakihusishwa na shambulio hilo baya katika hoteli ya DusitD2 . Lakini hawakusomewa mashtaka yao.

Mkurugenzi wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kufanya uchunguzi alioutaja kuwa mgumu na wa kimataifa.

Washukiwa wanne ni raia wa Kenya huku wa tano akiwa raia wa Canada mwenye mizizi ya Kisomali.,

Mapema maafisa wa polisi waliambia BBC waliwakamata watu saba.

Mtu mmoja ambaye alionekana na washukiwa hao kabla ya shambulio anaaminika kuwa miongoni mwa wale waliozuiliwa lakini hakuwasilishwa mahakamani mapema leo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad