Watanzania Watatu Wahukumiwa Jela Miaka 15 kwa Ugaidi Kenya
0
January 31, 2019
Wanzania watatu wamehukumiwa kwenda jela miaka 15 kila mmoja kwa kosa la kujihusisha na ugaidi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa VOA Swahili Walikamatwa 2018 wakivuka kuingia Somalia wakiwa na silaha zilizotumika kwenye vitendo vya kigaidi.
Vijana hao watatu kutokea visiwani Zanzibari ni Mbarouk Adibu (34), Idarous Abdirahman (32) na Islahi Juma (22).
Hukumu hiyo imekuja wakati serikali ya Kenya ikiongeza juhudi zake kupambana kupambana na ugaidi kufuatia shambulizi Sehemu ya Biashara na Hoteli mjini Nairobi uliouwa watu 21.
Tags