Watu wanne wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kupanga shambulio dhidi ya jumuiya ndogo ya Wiaslamu katika jimbo la New York.
Watu hao wanatuhumiwa kukutwa na mabomu ya kungeneza nyumbani na silaha za moto, na kupanga kushambulia jumuiya ya Islamberg iliyoanzishwa na kiongozi wa dini kutoka Pakistani kwenye miaka ya 80.
Njama hizo zilibainika baada ya polisi kupashwa habari na mwanafunzi.
Jumuiya ya Islamberg imekuwa ikilengwa na watu wenye misimamo mikali ambao wanadai imekuwa ikitumika kama kambi ya mafunzo kwa magaidi.
Watuhumiwa watatu Andrew Crysel, 18, Vincent Vetromile, 19 na Brian Colaneri, 20, wanatarajiwa kupandishwa mahakamani leo Jumatano.
Mnangagwa arejea nyumbani kwenye ghasia
Viungo sita vya mwili ambavyo havihitajiki tena na binadamu
Fahamu kazi 5 zinazolengwa na waajiri mwaka 2019
Wote wanakabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kinyume na sheria na kula njama.
Mtuhumiwa wa nne ni mvulana mwenye miaka 16.
Kwa mujibu wa polisi, watatu kati ya watuhumiwa hao walikuwa pamoja katika mafunzo ya uskauti.
Wapelelezi wanasema watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiishi katika jiji la Greece, kaskazini-magharibi mwa jimbo la New York walikuwa wametengeneza mabomu matatu na walikuwa na silaha 23 walizozificha katika sehemu tofauti.
Walikamatwa kwenye nyumbani kwao na mvulana mwenye miaka 16.
Mkuu wa police wa Greece Police Patrick Phelan amesema uchunguzi ulianza baada ya mtuhumiwa mwenye miaka 16 kusikika akiongelea njama zao na mwanafunzi mwenzake.
Jumuiya ya Islamberg inapatikana magharibi mwa milima ya Catskill karibu na jiji la Binghamton.
Jumuiya hiyo ambayo inaundwa zaidi na watu weusi ilihamia eneo hilo kukimbia uhalifu na wingi wa watu katika Jiji la New York.
Walinda amani wa UN wauawa Mali
Washukiwa wa ugaidi wajisalimisha, huku polisi wakitibua shambulio Kenya
Wakazi wa Greece wanasema watu wa jumuiya hiyo ni watu wa amani na marafiki, hata hivyo vyombo vya habari vya mrengo wa kulia kama Infowars vinadai bila ushahidi wowote kuwa jumuiya hiyo ni kambi ya mafunzo ya wanamgambo wa Kiislamu.
Mwaka 2017 Robert Doggart,kutoka jimbo la Tennessee, alifungwa jela kwa kula njama za kuchoma msikiti wa jumuiya hiyo.
Mwaka 2015, John Ritzheimer kutoka Arizona aliwatishia wanajumuiya hiyo kuwashambulia na silaha ya moto.
Watu wanne wanaswa kwa 'kupanga mashambulizi' dhidi ya Waislamu New York, Marekani
0
January 23, 2019
Tags