Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA, Hashimu Juma, amebainisha kwamba endapo chama chake kikipewa ridhaa ya kuongoza dola Rais hatakuwa na mamlaka na badala yake lazima atakuwa anafuata ushauri kutoka katika mabaraza ya wazee yatakayoundwa.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo amesema kwamba upo utafiti ambao wameufanya kama chama kwa kutazama nchi zilizoendelea na kugundua kwamba vipo vyombo ambavyo ndivyo vinakuwa na mamlaka na kwa CHADEMA wazee ndio watakuwa viongozi.
Ili kuimarisha nchi, Mzee Juma amesema, Baraza la Wazee litaundwa na wazee 100 huku wakitenga nafasi za Viti Maalumu Wabunge takribani 50 ili kuwawakilisha wazee nchi nzima.
"Mnaweza mkasema wote si watanzania mna kipi kipya, sisi CHADEMA tumefanya uchunguzi, wenzetu wanavyombo mbalimbali kama house of commerce nk. tutakuwa na Baraza la Wazee, Wizara ya Wazee na Wabunge wazee wa viti maalumu. Hawa ndiyo watakuwa wakiongoza nchi hii" Mwenyekiti Juma .
Ameongeza kwamba "Wazee 100 na wabunge 50 wakiungana atakuwa top na mwisho wa siku hawa ndiyo watakuwa wanaongoza nchi na maisha ya watanzania yatabaidilika na uchumi kuimarika", Juma.