Waziri Lugola azungumzia aliowatumbua kuendelea na kazi


Mapema leo kulichika taarifa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdun ameendelea kutekeleza majukumu ya cheo hicho licha ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutangaza kutengua uteuzi wake.

Waziri Lugola amesema bado hajapata taarifa za agizo lake kutotekelezwa ila alimtaarifi Mkuu wa Majeshi (IGP).

"Sina taarifa kwamba agizo langu halijatekelezwa, lakini nilimpa IGP muda wa utekelezajI, kwa hiyo naamini litatekelezwa. Saa nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka, na mimi ninayo. Utekelezaji unaendelea." amesema Waziri Lugola.

Utakumbuka January 16 mwaka huu Waziri Lugola ametengua uteuzi wa Makamanda wa polisi watatu ambao ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad