Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, amepiga marufuku tabia ya Maafisa Uhamiaji hasa waliopo mikoa ya mipakani kuwatambua Wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake.
Lugola amepiga marufuku hiyo Jana alipokuwa akiongea moja ya mikutano yake mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara yake ya kikazi iliyoanzia Januari 2, mwaka huu.
"Idara ya Uhamiaji kutambua wahamiaji haramu kwa kigezo cha pua ndefu, kuimba wimbo wa Taifa na urefu wa mwili wake nimepiga marufuku," alisema.
Aidha Lugola ameongeza kuwa Idara ya Uhamiaji ina taratibu na vigezo vyake kiweledi katika kushughulikia suala hilo, hivyo amesisitiza viendelee kutumika kubaini nani raia na nani si raia.