Wema Sepetu Apata Bahati Nyingine Ya Kuolewa


Msanii wa muziki wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amejikuta akipata bahati ya mtende Baada ya kijana mwingine ambaye anatajwa kuwa rubani kujitokeza kwa ajili ya kumuoa.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa rubani huyo anayekwenda kwa jina la Ham­dan Zakwani ‘Danzak’amejitosa kumuoa staa huyo ambaye ni Miss Tanzania 2006, kwa gharama yoyote.

Rafiki wa karibu wa Danzak ameliambia Gazeti hilo kuwa, siku nyingi Danzak alikuwa na ndoto za kufunga ndoa na staa huyo lakini hakupata muda wa kufanya hivyo kwa kuwa, alikuwa amebanwa na masomo.

Danzak alianza kumpenda Wema, kipindi kirefu sana na mara nyingi alikuwa akimfuatilia nyendo zake na kumpenda jinsi alivyo.

Baada ya kumaliza masuala yake ya kimasomo na kuajiriwa, ameamua kuja nyumbani kupumzi­ka kidogo na mimi nimekuwa kama mwenyeji wake, kwa sababu za­mani kabla hajawa rubani tuliwahi kufanya naye sanaa ya muziki”.

Gazeti la Ijumaa lilimsaka Wema ambaye hakutaka kauongelea Suala hilo Lakini Meneja Wake anayeitwa Neema Ndepanya amewataka wanaotaka kumuoa Wema waende nyumbani kwao kujieleza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad