Klabu ya soka ya Yanga imetoa jibu kwa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, aliyehoji juu ya utaratibu wa kuchangisha fedha kwa wanachama wake kama ni halali na unakatwa malipo ya kodi kwa serikali.
Kupitia ripoti yake ya michango ya fedha za mashabiki kwa miezi miwili ya Novemba na Desemba Yanga imeweka wazi kuingiza kiasi cha shilingi 5,165,009 kwa mwezi Desemba na 563,737 kwa mwezi Novemba.
Katika ripoti hiyo Yanga imeeleza michango hiyo imefanyika kwa njia ya simu kupitia Selcom Wallet hivyo lazima kodi zote sitahiki zitakuwa zimelipw
Makusanyo ya michango ya wanachama kwa njia ya Selcom kwa mwezi wa 11 na 12 mwaka 2018. Asanteni sana kwa michango yenu hii ndio maana sahihi ya timu ya wananchi. Daima mbele nyuma mwiko
Manara alihoji juu ya suala hilo hivi karibuni baada ya kusambaa video mtandaoni ikiwaonesha wachezaji wa Yanga wakipewa fedha na mashabiki baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa jijini Mbeya.
Yanga yamvaa Haji Manara Uchangishaji Fedha kwa Wanachama Wake
0
January 04, 2019
Tags