Ziara ya Tundu Lissu kuanza leo Ujerumani, kisha Marekani kwa siku 10


Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi katika nchi mbili za Ulaya na Marekani kuanzia siku ya leo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene amesema siku ya leo Lissu ataanza ziara yake nchini Ujerumani kwa siku mbili, ambako atakutana na baadhi ya maofisa wa Serikali pamoja na wabunge wa Bunge la Ujerumani.

Baadae Lissu atazuru Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji ambako atakutana na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, wabunge wa EU pamoja na wanadiplomasia wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao EU.

Baada ya Ubelgiji,  Lissu ataelekea Washington DC, Marekani kwa siku 10 ambapo mbali ya kukutana na Watanzania wanaoishi nchini humo atakutana pia na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na Watendaji wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID).

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad