Zitto aleta majibu ya Sakata la CAG na Ndugai
0
January 14, 2019
Mbunge Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amesema amepokea majibu kutoka kwa Katibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Akbar Khan kuhusu barua aliyomuandikia akimtaka kuingilia kati mzozo kati ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na-
Zitto ametoa kauli hiyo leo Januari 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za chama cha ACT-Wazalendo, Kijitonyama jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa CAG alikuwa akitoa maoni na maoni hayo yamemfanya Spika Ndugai kumtaka Profesa Assad kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ahojiwe na kujieleza siku ya Januari 21, 2019.
Profesa Assad anadaiwa kutoa maneno hayo, hivi karibuni wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kuhusu ukaguzi unaofanywa na ofisi yake kuonekana na wananchi kuwa haufanyiwi kazi na bunge na kuwa kwa kitendo hicho bunge ni dhaifu.
“Khan amenitaarifu barua yangu imefikishwa kwa Lifaka (Emilia-mwenyekiti wa CPA) ili aweze kushauriana na Ndugai namna bora ya kushughulikia migongano kati ya Bunge na CAG, nimetiwa moyo na hatua hii ya CPA kulifanyia jambo hilo kwa haraka inayostahili. Imani yangu Ndugai atazingatia heshima aliyojijengea CPA na kuepuka kuingia katika rekodi mbaya ya historia ya zaidi miaka 100 ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola", amesema Zitto.
Januari 9, 2019, Zitto alimuandikia Khan barua hiyo ambayo pia aliwatumia maspika wote wa nchi wanachama wa CPA na wanasheria wakuu, akieleza kuwa sakata hilo lilianza baada ya Profesa Assad kusema anaamini kuwa kutotekelezwa kwa ripoti anazozitoa, ni udhaifu wa Bunge.
EATV
Tags