Zitto Kabwe Ahofia Usalama Wake

Zitto Kabwe Ahofia Usalama Wake
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anahofia usalama wake kutokana na taarifa alizozipata, akisema kuna mpango wa kumdhuru.

Kiongozi huyo wa upinzani ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia agenda za muungano wa vyama 10 vya upinzani kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, alieleza kupitia mtandao wa Twitter, akionya wale walionuia kumdhuru.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe ameandika: “Tunafahamu kuwa Operesheni Maalumu #Mzizima2 imepewa kibali kutekelezwa. Dhima ‘ Vita ya Mwisho kuleta Nidhamu kamili’ inataka kinachoitwa kumnyamazisha SAI( mie huyo). Wakajipange upya Tu. Mungu tu Ndio anaweza kuninyamazisha. SIOGOPI mwanadamu mwenzangu aslani” alisema katika ukurasa huo.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. To be honest with you, i don’t know what is taking them very long

    ReplyDelete
  2. Ludi kwenu ukitaka kungangania kwetu sisi hatukutambui wala haupo KATIKA dhanna ya Raia mwema.
    We we NI mpotofu kibaraka WA Mabeberu.
    Ukweli WA kujiha. I unaujua mwenyewe.

    Umeyatafuta na Utayapata

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad