Afikishwa Mahakamani kwa kuomba rushwa ya mchele Kg.10 na Tsh. Mil. 1.5

Afikishwa Mahakamani kwa kuomba rushwa ya mchele Kg.10 na Tsh. Mil. 1.5
Mtaalamu wa mionzi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), Siriacus Mwombeki, amepandishwa Kizimbani katika mahakama ya Ilala, jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh. milioni 1.5 pamoja na mchele kilo 10 ili afanye upasuaji wa uvimbe katika goti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Ilala, Christopher Myava, Januari 31, mwaka huu alikamatwa na maafisa kwa kosa la kushawishi kuomba rushwa na kupokea rushwa kinyume cha sheria.

“Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na makosa ya kushawishi, kuomba na kupokea rushwa ya Sh.500,000 kinyume cha kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007,” alisema.

Myava alieleza kuwa Januari 28, mwaka huu Mwombeki akiwa kwenye majukumu yake alishawishi, aliomba na kupokea Sh. 40,000 ili kumsaidia mtoto Nangale Kazembe kwenye upasuaji wa uvimbe kwenye goti.

Alifafanua kuwa, Januari 28, mwaka huu Mwombeki alishawishi na kuomba Sh. 1,500,000 pamoja na mchele kilo 10 ili kumsaidia mtoto Kazembe afanyiwe upasuaji wa goti.

Ilidaiwa kuwa Januari 31, mwaka huu mtuhumiwa Mwombeki akiwa kwenye majukumu yake MOI, alipokea Sh. 500,000 kutoka kwa mzazi wa mtoto huyo, Kazembe Bundala, kama sehemu ya malipo ya fedha iliyoombwa ili kumsaidia mtoto wake kufanyiwa upasuaji wa goti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad