Afisa wa Takururu Mbaroni Kwa Kumbaka Mpwa Wake
0
February 12, 2019
Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Rukwa, Jonas Jackson (34) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kisha kumlawiti mtoto wa dada yake aliyekuwa akiishi naye
Alikamatwa Februari 7, 2019 baada ya mtoto huyo kwenda kuripoti kituo kikuu cha Polisi Mjini Sumbawanga kufuatia kuchoka kufanyiwa vitendo hivyo
Kamanda wa Polisi wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa jana Jumatatu Februari 11, 2019 baada ya mlalamikaji mwenye umri miaka 18, kwenda Polisi kutoa taarifa ya vitendo vya unyanyasaji anavyofanyiwa
Msichana huyo amedai kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo na mjomba wake tangu Septemba, 2018.
Tags