Ahukumiwa Miaka 30 Jela kwa Kumbaka Binti yake wa Kumzaa

Ahukumiwa Miaka 30 Jela kwa Kumbaka Binti yake wa Kumzaa
Mkazi wa kijiji cha Msigalile, Masasi mkoani Mtwara, Ally Katambo (30) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa) baada ya kuelezwa na Mganga wa jadi kuwa kwa kufanya hivyo, atapata utajiri.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Honorious Kando, alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kuanzia Juni Mosi hadi 29, mwaka jana akiwa nyumbani kwake kijiji cha Msigalile-Ndanda mjini Masasi.

Hakimu Kando alisema ushahidi ulitolewa na upande wa mashatka mahakamani hapo pamoja na mshtakiwa kukiri kufanya kosa hilo kwa madai kwamba ni kutokana na imani za kishirikina baada ya mganga wa jadi kwa lengo la kutaka utajiri na kutakiwa kufanya hivyo.

Alisema mahakama imemtia hatihani mshtakiwa na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa.

Kando alisema mtuhumiwa alikiri kuwa baada ya kuelezwa na mganga wake kufanya kitendo hicho, alirudi nyumbani na kumbaka mtoto wake ili kutekeleza masharti aliyopewa kwa lengo la kufanikisha azma yake.

Alisema kwa mujibu ya kifungu cha 158 (1) ( 2 ) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa makerebisho mwaka 2002, mahakama inamhukumu Katambo jela miaka 30 na kwamba hiyo itakiwa fundisho kwa jamii na watu wengine wanaofanya matukio kama hayo.

Katika kufikia uamuzi huo, Hakimu huyo alisema mahakama pia imejiridhisha na ushahidi wa vipimo vya kidaktari ambavyo vimeonyesha kuwa mtoto huyo amebakwa na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri, jambo ambalo pia limemwathiri kisaikolojia.

Baada ya hukumu, mahakama ilitoa fursa kwa mshtakiwa kujitetea na kuomba apunguziwe adhabu kwa vile kwa sasa ana watoto wawili wadogo na mke mmoja ambao wanamtegemea kimaisha.

Awali, mwendesha mashtaka wa polisi, Koplo Selemani, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine na jamii kwa ujumla, na kwamba kwa kumbumbuku za nyuma za mshtakiwa hakuwa na kosa lolote alilowahi kulifanya isipokuwa hilo la ubakaji.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad