ALERT: Kolabo kubwa mbili zinakuja, Diamond ft Harmonize na Ommy Dimpoz ft Alikiba
0
February 16, 2019
Kama wewe ni shabiki au mdau wa muziki wa Bongo Fleva, basi mwaka huu utauanza vizuri kwani kuna kolabo kubwa mbili zinakuja za wasanii wakubwa hapa Tanzania.
Kolabo ya kwanza ni ya Ommy Dimpoz na Alikiba, tayari wawili hao wameshaingia locations nchini Oman ku-shoot video ya kolabo hiyo.
Hii ni kolabo ya tatu ya wawili hao, ambayo watu wengi wanaisubiri kwa hamu baada ya kolabo zao mbili za wimbo wa Nai Nai na Kajiandae kufanya vizuri.
Kolabo nyingine kubwa inayosubiriwa kwa hamu ni ya Diamond Platnumz na Harmonize.
Hii inakuwa ni kolabo ya tatu kwa wasanii hao kutoka WCB, hii ni baada ya kufanya vizuri na kolabo mbili za Bado na Kwangwaru.
Tags