Aliyeachiwa kwa Msamaha wa Rais Akamatwa na sare za JWTZ Dar

Aliyeachiwa kwa Msamaha wa Rais Akamatwa na sare za JWTZ Dar
Jeshi la Polisi Kanda ya maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Emmanuel Joseph Magoti kwa kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa mfungwa katika gereza la Segerea na aliachiwa kwa msamaha wa Rais mwaka jana.

"Lengo lao ni kujificha kwenye mavazi haya ili lolote wanalolitenda nilielekezwe kwa jeshi la wananchi wa Tanzania, jeshi ambalo linaheshima kubwa na linafanya kazi kwa mujibu wa sheria," amesema.

Aliendelea kwa kusema, 'Nichukue nafasi hii kumpongeza mwananchi mwema ambaye alitupa taarifa kuhusu kuwepo kwa muhuni huyo na wenzake ambao walifanikiwa kukimbia,'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad