Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Simon Ngatunga pamoja na Afisa Rasilimali Watu, Fredy Muhochi wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na jumla ya makosa matatu.
Kati ya Juni 16 hadi 20, 2017 washitakiwa waliandika dokezo la shilingi milioni 2.9 linaloeleza kuwa mshitakiwa wa kwanza anastahili kulipwa kiasi hicho kama posho ya simu na umeme wakati haikuwa kweli.
Katika shitaka la pili linalomkabili mshitakiwa wa kwanza pekee, Simon Ngatunga, ilidaiwa kuwa alifanya ubadhilifu wa kiasi cha shilingi milioni moja na laki nne.
Shitaka la tatu linalomkabili mshitakiwa wa pili Fredy Muhochi ilidaiwa na wakili Mashingia kuwa mshitakiwa alimsaidia mshitakiwa wa kwanza kuandaa dokezo la mshitakiwa wa kwanza kustahili kulipwa kiasi cha shilingi milioni 2.9 kwa ajili ya posho ya umeme na simu.
Ngatunga aliyekuwa Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge tangu mwaka 2016 alipoteuliwa kwa mara ya kwanza, uteuzi wake ulitenguliwa mwaka jana mwezi wa nane na Rais John Magufuli