Baada ya Taharu Bungeni, Wabunge Warejea Ndani ila Bado chanzo cha Alarm Kulia Hakijajulikana



Saa moja baada ya kikao cha Bunge kuharishwa kutokana na taharuki iliyotokana na ving’ora kulia, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema mpaka sasa hawafahamu chanzo cha tukio hilo.

Kabla ya kuahirishwa kwa kikao cha Bunge saa 5:03 asubuhi kilikuwa kikiongozwa na mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga.

“Nawapeni pole. Hadi sasa hivi hatujajua chanzo tutakapojua tena baadaye tutaelezana sababu ya kulia kwa ving’ora,” amesema.

Amesema kama kuna maswali (ya wabunge) yamebaki watayafanyia utaratibu huku akiwapa pole wabunge na kwamba wataalamu wanaendelea kufanya uchunguzi.

Licha ya wabunge kuambiwa waingie ndani ya ukumbi saa 5:31 asubuhi lakini kikao kilichelewa na kuanza saa 6:03 mchana.

“Kulikuwa kumebakia maswali mawili hayajajibiwa,” amesema Ndugai na kuongeza: “Tutayafanyia utaratibu siku zijazo.”

Wenyeviti wa kamati wanaosoma taarifa zao wameambiwa wasome kwa dakika 30 kila mmoja badala ya dakika 45.

Na Sharon Sauwa, Mwananchi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad