Baba Nandy Afunguka 'Video ya NANDY ilivyovuja Nilisema Huu Ndio Mwisho wa Huyu Mtoto'

Wazazi wa Nandy wafunguka sakata la video ya utupu

Baba Mzazi wa msanii Nandy amefunguka kuhusu tukio la aibu alilowahi kulifanya binti yake la kuvuja kwa video yake ya utupu na msanii Billnass, na kusema kwamba lilimtia aibu sana kwenye jamii.


Akizungumzia hilo Baba Nandy amesema kwamba siku iliyovuja video hiyo alikuwa akipigiwa simu kila dakika kumlaumu kwa kitendo chake cha kumuacha mtoto afanye sanaa, licha ya ndugu zake wengi kutofurahishwa na suala hilo.

Baba Nandy ameendelea kusema kwamba alipopata taarifa juu ya kilichojiri, alitaka kumpiga marufuku Nandy kuendelea na muziki, huku akisema kwamba jambo hilo ndio mwisho wake wa kila kitu kuhusu maisha ya sanaa.

“Nilikuwa ofisini kwangu napigiwa simu nyingi nyingi wananilaumu vipi mtoto, yaani kama vile kitendo alichokifanya Nandy ni kama nimekifanya mimi, kwa jinsi wanavyotoa shutuma, nikawa najiuliza kumetokea nini, katika kuchunguza ndio nikaambiwa, mimi sijaiona hiyo picha, niliambiwa tu, nilichokifanya nikasema huu ndio mwisho wa huyu mtoto, mwisho wake wa kuimba umefika, sababu yale niliyokuwa nayaogopa naona yameshakuja”, amesema Baba yake Nandy.

Sambamba na hayo, naye mama mzazi wa msanii huyo amesema kwamba tukio lile lilimpa wakati mgumu, kwani alishindwa hata kula na kumfanya akae njaa kwa siku tatu, na kusema kwamba iwapo atarudia kufanya vile basi huenda akapoteza maisha kabisa.

“Nilikuwa sipokei simu kwa sababu nilikuwa najua nitakachoulizwa, nilikosa raha nilikaa siku tatu sijala kitu zaidi ya kunywa chai tu, alipokuja kuona alizimia akashtuka yuko hospitali, lakini ni mateso, sikufichi ni mateso, Nandy siku akirudia naweza nikafa kabisa”, amesema Mama Nandy.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2018 ulikuwa mwaka mgumu kwa msanii huyo baada ya kuvuja kwa video yake ya utupu akiwa faragha na msanii mwenzie Billnass.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad