Bandari Mpya yajengwa Muleba


Mamlaka ya Bandari (TPA) imejenga bandari ndogo katika Mwalo wa Magarini katika halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera, iliyogharimu Shil 2.5 bilioni kwa ajili ya kuongeza ukusanyaji mapato ya serikali wilayani humo.

Hayo yamesemwa na mbunge wa Muleba Kusini Profesa, Anna Tibaijuka ambapo amesema kuwa halmashauri inatumia bandari hiyo iliyojengwa Mwalo wa Katunguru kuongeza mapato ya ndani kila mwaka

”Bandari hiyo na iliyojengwa na halmashauri ya wilaya katika Mwalo wa Katunguru, zinaongeza mapato yanayoboresha huduma za kijamii pia kuimarisha doria zinazodhibiti uvuvi haramu” Amesema Tibaijuka

Aidha, wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria majini wilayani humo wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwapunguzia ushuru wa tozo ya Shil. 3.6 milioni kwa mwaka ya kusafirisha abiria kwenda visiwani na kurudi ili wasipitie njia za panya

Kwa upande wake, Katibu wa kikundi cha wamiliki wa vyombo hivyo, Masudi Ibrahimu amesema tozo inayochukuliwa na halmashauri kila siku ni Sh. 10,000 kwa boti moja haiendani na mapato kwa wamiliki wa vyombo hivyo na wanaweza kufilisika.

Naye Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi, Richard Ruyango amezindua kikundi hicho katika Mwalo wa Magarini wilayani humo huku akiwataka wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria majini kufanya kazi kwa kulinda usalama wa wateja wao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad