BREAKING: Waziri Mwakyembe aagiza kukamatwa Dudu Baya kwa kumdhihaki Ruge


Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amelielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua Msanii Dudu Baya kwa kumdhihaki Marehemu Ruge Mutahaba.

Msanii Dudu Baya amekuwa akitumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutoa lugha isiyifaa kimaadili kwa Marehemu Ruge Mutahaba.

Ruge Mutahaba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG)amefariki siku ya jana nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad