Bunge lashauri michezo ya kubahatisha iongezwe kodi


Serikali imeshauriwa kuongeza kodi kwenye mapato anayopata mchezaji kwenye michezo ya kubahatisha  ili kupata mapato zaidi na wakati huo kupunguza ushiriki.

Ushauri huo ulitolewa jana bungeni na Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti, George Simbachawene wakati akiwasilisha taarifa ya mwaka kuhusu utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha Januari 2018 hadi 2019 pamoja na tathimini ya utekelezaji wa bajeti kipindi cha nusu mwaka 2018/19.

Simbachawene alisema michezo ya kubahatisha imekuwa ikikua kwa kasi sana nchini huku asili yake ikiwa si ya kiuzalishaji hivyo haina mlolongo wa thamani ambapo ina madhara makubwa kwa Taifa.

Alisema serikali inaweza kuweka kiwango cha dau la chini ambalo mshiriki atapaswa kuwa nalo ili aweze kushiriki michezo hiyo.

Alisema hatua hiyo ni kinyume na ilivyo hivi sasa ambapo kiwango cha chini ni sh. 500 ambacho hata mtoto chini ya miaka 18 anaweza kupata.

“Kamati inashauri  Serikali kuendelea kuongeza kodi kwenye mapato  anayopata mchezaji  ili kupata mapato zaidi  na wakati huo huo kupunguza ushiriki,’alisema.

Simbachawene ambaye ni Mbunge wa Kibakwe(CCM) alisema  Serikali inaweza kuweka kiwango cha dau la chini ambalo mshiriki atapaswa kuwa nalo ili mshiriki aweze kushiriki michezo hiyo kinyume na ilivyo sasa ambapo kiwango cha chini ni shilingi 500 ambacho hata mtoto anaweza kukimudu,”alisema.

Akichangia taarifa hiyo,aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage ambaye ni Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage (CCM) aliunga mkono  kuongezwa kwa kodi katika michezo hiyo

Mwijage alisema kwa kiasi kikubwa michezo ya kubahatisha imeleta uzezeta katika jamii na watu kushindwa kufanya kazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad