Burundi imetishia kuoyaondoa majeshi yake Somalia

Burundi imetishia kuoyaondoa majeshi yake Somalia
Burundi imetishia kuondoa wanajeshi wake 5,000 nchini Somalia ambako wamekuwa wakihudumu chini ya kikosi cha kulinda amani cha Muungano wa Afrika, AMISOM kufikia mwisho wa mwezi huu.

Muungano wa Afrika umeitaka Burundi kuwaondoa wanajeshi 1000 kutoka kikosi cha AMISOM kufikia mwisho wa mwezi huu hatua ambayo serikali ya Burundi inapinga.

Waziri wa ulinzi Emmanuel Ntahomvukiye, amewaambia wabunge kuwa serikali tayari imetoa ilani kwa AU kuhusiana na suala hilo.

''Tunatemewa mate, tunafanywa kama sisi sio Wakenya''
Ni mataifa gani yaliohalilisha na kupinga mapenzi ya jinsia moja
Kwa nini Beyonce na Jay-Z walipiga picha mbele ya picha ya Meghan Markle?
Mataifa matano ya Afrika yanachangia wanajeshi wao katika kikosi cha kulinda amani cha AMISOM nchini Somalia.

Japo kuna hofu kuwa taifa hilo la upembe wa Afrika bado linakabiliwa na tishio kutoka kwa kundi la Al Shabab.

Chini ya makubaliano ya Umoja wa mataifa ni kuwaondoa zaidi ya wanajeshi elfu ishirini wa kulinda amani wanatakiwa kuondoka kwa awamu ili kuipokeza majeshi ya Somalia usukani wa ulinzi wa taifa lao.

Ufadhili umetajwa kuwa changamoto kubwa kwa vikosi vinavyolinda usalama inchini Somalia.

Kila mwezi zaidi ya wanajeshi elfu ishirini wanaohudumu chini chini ya jeshi la pamoja la muungano wa afrika AMISOM, wanalipwa zaidi ya dola elfu moja kila mmoja.

Mshahara wao umekuwa ukilipwa na Muungano wa Ulaya moja kwa moja kupitia mataifa yao kwa kutumia sarafu za kigeni.

Wafahamu wapiganaji wa al-Shabab kutoka Somalia
Kenya na Somalia zateta kuhusu visima vya mafuta
Wanajeshi hao hata hivyo hulipwa mishahara yao kwa sarafu ya nyumbani.

Serikali ya Burundi haioni kwanini mpango wa sasa wa AU wa kupunguza wanajeshi katika kikosi hicho unalenga wanajeshi wake pekee.

Sio mara ya kwanza Burundi kutishia kuwatoa wanajeshi wao kutoka Amisom lakini hatua hii ya sasa huenda ikawa na athari kubwa.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Mwaka 2017 Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alitangaza kuwa serikali yake itaishtaki Muungano wa Ulaya kuwa kuzuia mshahara wa vikosi vya Burundi vilivyoko nchini Somalia kwa karibu mwaka mmoja.

''Tatizo liliko kwa sasa ni kwamba kikosi cha Amisom hakina ufadhili iliyokuwa nao hapo awali baada ya Muungano wa Ulaya EU kujiondoa sasa mataifa ambayo yanachangi kikosi hicho yanalazimika kkugharamia uwepo wa majeshi yao'' anasema mtaalamu wa masuala ya usalama nchini Kenya George Musamali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad