Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) kimelitaka Jeshi la Polisi nchini kufanya kazi kwa weledi na kuacha kukurupuka katika utendaji kazi wake.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo na kudai jeshi hilo limekuwa likikiuka weledi wao wa kazi na kukamata viongozi na wabunge wa chama hicho kwa kutumia mabavu.
Aidha, Mwalimu amedai kilichozungumzwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi katika mkutano wake jijini Mbeya hakukuwa na viashiria vyovyote vya ukiukwaji wa sheria na kudai kuwa kilichpfanywa na jeshi hilo ni kutumia nguvu kwa kuwaminya wanaopinga maagizo ya Rais.
Jana, Februari 21, 2019, Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya lilimshikilia Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, kujibu madai ya kutoa kauli ya uchochezi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC) Urich Matei, ni kwamba Sugu ameonekana katika moja ya clip za video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akisikiliza hoja na malalamiko ya wananchi na kuyatolea ufafanuzi na ndipo alipoongea kwa kutoa msimamo wake kuhusu zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo-wadogo (wamachinga) na kusema havifai na vinastahili kuchomwa moto.
Chadema Waingilia Kati Sakata la Sugu Wawataka Polisi Wasikurupuke
0
February 22, 2019
Tags