Wamiliki wote wa daladala wanaotumia kituo cha Gerezani wamepewa siku mbili kutakiwa kuondoa gari zao ndani ya kituo hicho ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo Kasi (DART).
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya DART iliyotolewa leo Februari 7, ujenzi huo utahusisha barabara ya Kilwa kuanzia katikati ya Jiji la Dar es salaam hadi Mbagala Rangi Tatu na barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni, Barabara ya Chang'ombe, Mgulani hadi makutano ya barabara ya Kilwa na eneo la Mgulani JKT.
Aidha katika hatua nyingine, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, imetoa utaratibu utakaotumika kwa safari za daladala zilizokuwa ziantumia kituo hicho, kama inavyoonekana hapo chini.
Daladala zapewa siku 2 Kuondoka Kituo cha Gerezani Kupisha Ujenzi wa Barabara za Mwendokasi Mbagala
0
February 07, 2019
Tags