Msanii wa filamu nchini, Mwijaku amesema ni wazi kuwa Diamond Platnumz alimdanganya
mpenzi wake, Tanasha kuwa angemuoa siku ya wapendanao (valentine Day).
Mwijaku ambaye amekuwa maarufu mtandao hivi karibuni kutokana na kuzungumzia na kuchambua
masuala ya mahusiano, amefunguka hayo alipokuwa akihojiwa na Wasafi TV.
"Diamond amemdanganya mpenzi wake kwa sababu alimuahidi atamuoa lakini akampelea maua na
maragi rangi mekundu, mwanamke naye akakubali," amesema.
"Ebu pata picha unatoka kwenye dhamani ya ndoa unakuja kupewa maua mekundu halafu
unafurahia?. Hii ni ishara tosha wanawake wametoka kwenye ubavu wetu," amesitiza Mwijaku.
Mwishoni mwa mwaka jana msanii Diamond Platnumz alitangaza kuwa angeoa February mwaka huu, na mpenzi wake wa sasa Tanasha kutokea nchini Kenya ndiye aliyekuwa akitajwa kuhusika zaidi kwenye ndoa hiyo.