Dude Awatolea Povu Wanaomponda Rais

Dude Awatolea Povu Wanaomponda Rais
Msanii wa bongo movies Kulwa Kikumba amefunguka na kuwakanya wale wote ambao wamekuwa na tabia ya kumsema vibaya Mh Rais kutokana na jitihada anazozifanya huku wakisema kuwa hakuna jipya na la maana.

Msanii huyo ameyasema hayo leo alipokuwa katika moja ya safari waliopangiwa na Mh mkuu wa mkoa , baada ya wasanii hawa kupewa ofa hiyo ya kutembelea miundombinu hasa ujenzi wa reli ya kisasa ya Morogoro hadi Dar Es Salaam.


Dude aasema kuwa kwa kile alichokiona kikiendelea hapo anaona kabisa juhudi kubwa za Mh Rais na amekuwa akiwashangaa sana wale ambao wamekuwa akisema kuwa mh hafanyi kazi yoyote.

Hata hivyo Dude ametoa wito kwa wasanii wote nchi kuwa mabalozi wa maendeleo na kutangaza mema ambayo Rais amekuwa akiyafanya kwa wananchi wake.

Dude pia ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wasanii wote kuwa na umoja na  mshikamano kwa kila kitu hasa katika kufanya kazi na kuacha ubaguzi ambao mwisho wa siku hauna tija yoyote.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad